Na Mariam Muhando_Dar es salaam.
KATIBU wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzi wa Chama Cha Mapinduzi CCM CPA Amos Makala amempongeza Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli Kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuhakikisha changamoto zinatatuliwa Jimboni humo.
Makala ameyabainisha hayo katika Mkutano uliowakutanisha Wananchi wa Jimbo la Segerea mara baada ya kufanya Ziara Jimboni humo Kwa lengo la kusikiliza kero na kuzipatia Ufumbuzi sambamba na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.
“Huyu mama ni Kamanda Mzuri anaekaa na Wananchi wa Jimbo hilo katika kuhakikisha Maendeleo yanapatikana Segerea,” amesema Makala.
Wakati huo huo amemuahidi Mbunge wa Jimbo hilo Bonnah kuwa ataendelea kumuunga mkono Ifikapo julai nane mwaka huu Wananchi Wanaokabiliwa na changamoto ya kutolipwa fidia ya bomoa bomoa wanalipwa.