Home KITAIFA DCI KINGAI AKABIDHI VYETI VYA HESHIMA NA ZAWADI KWA ASKARI WALIOFANYA KAZI...

DCI KINGAI AKABIDHI VYETI VYA HESHIMA NA ZAWADI KWA ASKARI WALIOFANYA KAZI VIZURI ZAIDI DAR ES SALAAM

Dar es Salaam

MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini Kamishna wa Polisi Ramadhani Kingai leo Julai 9, 2024 Katika ukumbi wa Maofisa wa Polisi uliopo Oystabey Kinondoni amewakabidhi vyeti vya heshima askari 13 wa Jeshi la Polisi waliofanya kazi vizuri zaidi kwa mwaka 2023/2024.

CP. Kingai amesema askari hao wamepewa vyeti na zawadi hizo kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Jeshi la Polisi (Police General Orders) na Kauli mbiu ya Jeshi la Polisi ya Nidhamu, Haki weledi na uadilifu.

“Nimewatunuku vyetu askari 13 wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ambao hawa wachache wanawakilisha wenzao, askari wanaofanya vizuri ni wengi ambao ni wazuri pia.” asema CP Kingai.

“Vyeti na zawadi hizi zinalengo la kuwapa motisha na morali askari wengine kujituma zaidi ili nawao watambulike,” CP Kingai ameongezea.

Katika hatua nyingine CP . Kingai amesema kuwa hali ya usalama nchini imeimarika kutokana utendaji mzuri wa askari kama hawa waliopewa vyeti.

Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Denis Simbeye kwa niaba ya waliopewa zawadi ameshukuru kwa kutambuliwa mchango wao na kuahidi kuwa ataendelea kuimarisha nidhamu ya utendaji kazi na cheti alichopewa kitakuwa hamasa hata kwa askari wengine ili waweze kufanya vizuri zaidi.

Zoezi hili la kuwatambua askari waliofanya vizuri zaidi hufanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu jumla ya askari 13 wametambuliwa na kupewa vyeti na zawadi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here