Iringa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku 23 kwa Wizara za Ujenzi, Uchukuzi, taasisi zinazosimamia sekta ya anga na uongozi wa mkoa wa Iringa kutatua vikwazo vilivyopo ili uwanja wa ndege wa Iringa uanze kutumika ifikapo Agosti mosi, mwaka huu.
Ametoa agizo hilo leo Julai 8, 2024)wakati akizungumza na viongozi na wananchi mbalimbali waliokuwepo uwanjani hapo mara baada ya kukagua ujenzi wa uwanja huo. Gharama za ujenzi wa uwanja huo ni shilingi.bilioni 63.7 na gharama za usimamizi ni sh. bilioni 1.1.
“Nimesema Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi, TAA, ATCL, Mamlaka ya Hali ya Hewa, TANROADS na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa wakae, wafanye vikao na kuondoa vikwazo kabla ya tarehe 30 Julai ili ifikapo tarehe 1 Agosti, 2024 uwanja huu uanze kufanya kazi,” amesema.