Home KITAIFA SERIKALI INAENDELEA KUWEKEZA UJENZI WA VYUO LENGO KUTOACHA NYUMA WATU

SERIKALI INAENDELEA KUWEKEZA UJENZI WA VYUO LENGO KUTOACHA NYUMA WATU

DAR ES SALAAM

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka Elimu na Mafunzo Stadi (VETA) ,CPA Anthony Kasore amesema serikali imeendelea kuwekeza Ujenzi wa vyuo kuanzia Wilaya hadi Mikoa ikiwa na lengo ya kutoacha nyuma watu wote kwenye kupata mafunzo ya ujuzi.

Hayo yamebainishwa Julai, 6 2024 na CPA Kasore alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.amesema kuwa katika maonesho hayo kuna Ubunifu wa Teknolojia mbalimbali ambazo zinakwenda kutatua changamoto katika sekta zote za kiuchumi.

CPA Kasore amesema kuwa vijana wa Tanzania katika maeneo yote wajitokeze kwenda katika vyuo vya VETA kwani vimejengwa waende wapate mafunzo ya ujuzi ambapo watakuwa wameondokana na tatizo la ajira kutokana na fursa zilizopo katika maeneo yao

Pia CPA Kasore ametoa wito kwa jamii kuacha kuwafungia watu wenye mahitaji Maalum na badala yake wawapeleke VETA kupata ujuzi wa aina mbalimbali.

Aidha amesema kuwa Serikali ya Chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imevutia wawekezaji wengi ambapo nguvu kazi hiyo Uwekezaji itatoka VETA.

Amesema kuwa baada ya kutambua kuwa kuna uwekezaji mkubwa wa viwanda wameanzisha fani ya Mechatronics ambapo wanaosomea kozi hiyo watakwenda huko kutokana na mitambo ya viwanda kuhitaji wataalam hao.

Amesema inataka vijana wote nchini wapate ujuzi ambao unakwenda kuwa fursa yao katika kuendesha maisha yao .

Ameongeza kuwa wanakwenda na Sera ya Serikali ya kuwa wanafunzi wote wanafika kidato cha nne ambapo watapata kusoma mafunzo ya ujuzi hapo ndipo VETA kuwa na kutengeneza Walimu watakwenda kuwafundisha ujuzi.

Amesema kuwa Kilimo ni Uti wa mgongo ambapo wanaotaka kufanya Kilimo watapata mafunzo na ujuzi na Kilimo cha uhakika na sio Kilimo cha kubahatishaa hali kadhalika kwa Sekta mifugo na Uvuvi wafanya hivyo hivyo.

CPA Kasore amesema kuwa Hadi wastaafu wanaweza kupata mafunzo ya ujuzi na kuweza kuendelea kuzalisha bila kutegemea mafao ya ustaafu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here