Home AFYA MENEJIMENTI YA MOI YARIDHISHWA NA HALI YA UTOAJI WA HUDUMA ZA MOI...

MENEJIMENTI YA MOI YARIDHISHWA NA HALI YA UTOAJI WA HUDUMA ZA MOI SABASABA.

Dar es Salaam 

MENEJIMENTI ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeridhishwa na hali ya utoaji wa huduma ya ushauri na elimu ya matibabu ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu katika banda la MOI kwenye maonesho 48 ya biashara ya kimataifa ya Sabasaba.

Menejimenti ya Taasisi ya MOI imetembelea banda la MOI leo Julai 8, 2024 katika maonesho hayo ya Sabasaba ili kujionea hali ya utoaji wa huduma za MOI kwa wananchi.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Orest Mushi amesema hali ya utoaji huduma za MOI kwa wananchi ni nzuri, ambapo zaidi ya wananchi 1,200 wamepata huduma katika banda la taasisi hiyo

“Leo tumekuja katika banda letu la MOI hapa Sabasaba kwaajili ya kujionea huduma zetu tunazotoa kwa wananchi wetu, banda letu linatoa huduma za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kwa wananchi ambapo mpaka sasa zaidi ya wagonjwa 1,200 wameshaonwa na kuchunguzwa pia zaidi ya wagonjwa 300 wamepewa rufaa ya kuja MOI ili wapate matibabu zaidi,” amesema Mushi

Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kufika banda la MOI ili kupata ushauri bure juu ya lishe bora, vipimo mbalimbali vya magonjwa ya mifupa, ubongo na mgongo pamoja na viungo bandia.

Naye, Mkurugenzi wa huduma za uuguzi wa MOI, Fidelis Minja amesema Taasisi ya MOI imejipanga vizuri kuwapokea wagonjwa wote waliopewa rufaa ya kwenda kupata matibabu katika taasisi hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here