Home KITAIFA KUIMARIKA KWA SEKTA BINAFSI KUTASAIDIA KUONGEZA AJIRA KWA VIJANA.

KUIMARIKA KWA SEKTA BINAFSI KUTASAIDIA KUONGEZA AJIRA KWA VIJANA.

Na Esther Mnyika,Dar es Salaam

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Suleiman Jaffo amesema kuimarika kwa sekta binafsi kutasaidia kuongeza ajira kwa vijana wanaohitimu elimu ya juu nchini.

Hayo ameyasema leo, Julai,6 2024 Dk. Jaffo wakati alipohudhuria Siku maalum ya China iliyoambatana na maonesho ya 48 ya biashara ya kitaifa -Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Amwakaribisha wawekezaji kutoka China na mataifa mengine kuwekeza ili kukuza uchumi na kutoa ajira kwa vijana.

“Taarifa inaonesha kwamba zaidi ya dola za Marekani bilioni 3.3 tunasafirisha , lakini tunaingiza bidhaa kutoka China ambazo thamani yake ni zaidi ya shilingi trilioni 3.5,”amesema.

Amesema Tanzania na China zinauhusiano wa muda mrefu ambayo yemeleta faidi katika nchi hizo hasa katika uchumi kwa kusafirisha bidhaa.

Ameongeza kuwa uhusiano mwingine upo kwenye viwanda vya wachina ambavyo vimejengwa hapa nchini na kutoa ajira nchini,ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa kufanya kazi ya ukandarasi.

Amesema kampuni 100 zimeweza kushiriki katika maonesho hayo ua 48 ya biashara ya kimataifa.

“Makampuni hayo yametoka China, hii tunavutia uwekezaji katika nchi yetu, binafsi kama Serikali imeamua inaweka mazingira wezeshi kuhakikisha wawekwzaji wanapata fursa ya kuwekeza nchini,”amesema.

Dk. Jaffo amehamasisha kuendelea kwa ushirikiano huo na kuwekeza ili kukuza uchumi na kuongeza ajira kwa vijana.

Amesema vijana wengi wanamaliza vyuo vikuu ambapo serikali haiwezi kuajiri vijana wote .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here