Home KITAIFA NAIBU KATIBU MKUU ZUHURA YUNUS ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU

NAIBU KATIBU MKUU ZUHURA YUNUS ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU

Dar es Salaam

NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus ametembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar Es Salaam leo Julai, 52024.

Aidha, amehimiza watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea kutatua changamoto za wananchi wanaotembelea banda hilo kwa ajili ya kupata huduma na uelewa masuala yanayotekelezwa na ofisi hiyo.

Katika Maonesho hayo Naibu Katibu Mkuu ametembelea Idara, Vitengo na Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kujionea namna huduma zinavyotolewa kwa wananchi na wadau wanaotembelea banda hilo katika maonesho hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here