Home KITAIFA MAONESHO YA 48 77 TANZANIA IMEPIGA HATUA KWENYE MATUMIZI YA TEKNOLOJIA

MAONESHO YA 48 77 TANZANIA IMEPIGA HATUA KWENYE MATUMIZI YA TEKNOLOJIA

Esther Mnyika, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu Kiongozi, Dk. Mosses Kusiluka amesema maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara ya mwaka 2024 yameonesha Tanzania imepiga hatua kwenye ukuaji na matumizi ya teknolojia.

Hayo ameyasema Leo Julai 4 2024 wakati alipotembelea maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayifanyika katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.

Amesema katika maonesho hayo, teknolojia nyingi zilizopo zimefanyiwa hapa nchini.

“Watanzania wenyewe tumebadilika, tumechangamka kuwa wabunifu na kukumbatia teknolojia mpya naona fahari kuwa Mtanzania.

“Hata teknolojia za nje zinakuja kwasababu wanajua kuna watu watashirikiana nao ,inawezekana ukaja bila wazo ukapata wazo la kibiashara,”amesema.

Amesema mwaka huu kuna washiriki wengi ukilinganisha na maonesho ya mwaka jana ambapo ushiriki wa wenyeji ni zaidi ya 3200 na wageni wakiwa zaidi ya wafanyabiashara 400.

“Tumejionea mambo mengi tumepita kwenye mabanda ya uzalishaji bidhaa mbalimbali, watoa huduma tumeangalia teknolojia na ubunifu,”amesema.

Amesema mabanda ya nchi mbalimbali yapo kwenye maonesho hayo ikidhihirisha hayo ni maonesho ya kimataifa yanazidi kukua ikionesha nchi inazidi kukua inaaminika.

Amesema nchi itapata fursa ya kuonesha bidhaa nchi zingine.

Amewahamasisha Watanzania kushiriki katika maonesho hayo ili kuona mabadiliko ambayo yapo ukilinganisha na maonesho ya mwaka jana.

“Kuona ni kuamini, sote tunafahamu ufunguzi umefanyika Rais wa Jamhuri ya Msumbiji alikua mgeni rasmi kwenye ufunguzi akiambatana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.Nawakaribisha Watanzania wote waje kuona maonesho haya,”ameongeza.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara amesema maonesho ya mwaka huu nchi mbalimbali za kimataifa zimeweza kushiriki nchi 26.

Amesema kampuni mbalimbali kutoka nje ya nchi zimeshiriki zaidi ya 400 na washirika wa Tanzania zaidi ya 3000 katika kuhakikisha maonesho hayo yanafanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Amesema wanavyofanya maonesho
makubwa kama hayo maana wameleta taasisi za kimataifa zinazojishughulisha na masuala la kibiashara hivyo wapo wakezaji wakubwa.

“Muwekezaji wa Kitanzania na mfanyabiashara atakutana na wawekezaji wa nje kubadilishana uzoefu hivyo nchi 26 zipo ndani ya sabasaba atakutana na wawekezaji wa kimataifa zaidi ya 400,” amesema

Ameongeza kuwa wakiwa na mratibu mzuri wa serikali ofisi ya waziri mkuu shughuli zote zinalatibiwa chini ya Waziri mkuu zipo kwenye maonesho hapo kuna kliniki ya biashara na taasisi za kiserikali akingia hapa anapata huduma zote.

Amesema wanatarajia maonesho hayo kuendelea hadi Julai 13 ambapo Rai wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk.Hussein Ali Mwinyi kufunga

Aidha ametoa wito kwa wafanyabiashara na wananchi kupata fursa zilizopo ndani ya maonesho hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here