Home KITAIFA FARAJA: MHITIMU WA VETA ALIYEAMUA KUANZISHA KIWANDA CHAKE

FARAJA: MHITIMU WA VETA ALIYEAMUA KUANZISHA KIWANDA CHAKE

Dar es Salaam

MHITIMU wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dodoma, Faraja Michael wa fani ya uchomeleaji,ameanzisha kiwanda chake cha kutengeneza vitu mbalimbali vinavyotokana na chuma pamoja na Aluminium.

Akizungumza leo Julai, 5 2024 katika Banda la VETA kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (DITF) maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Michael amesema kuwa katika maisha na elimu yake ya Darasa la Tatu tu hakuwahi kufikiria kuja kuwa na kiwanda lakini kutokana na mradi E4DT ameweza kuanzisha kiwanda cha uchomeleaji.

“VETA imeweza kuniinua kama kijana kupata ajira yangu ya kudumu inayotokana na ujuzi licha ya kuwa darasa la tatu B,” amesema Michael.

Amesema kuwa ujuzi alioupata sasa anaendesha maisha yake na kuondokana na tatizo la ajira.

Amesema kazi kubwa katika ujuzi ni kujituma na kuangalia kitu cha ziada ambacho jamii inahitaji lakini hawezi kupata.

Aidha amesema kuwa vijana wengi wanasema hakuna ajira wakati wakisoma VETA ajira hizo watapata kupitia ujuzi wao.

Pia amesema VETA ina fani zote ambazo kijana yeyote anaweza kuzifikia lakini kwa kuweka nia yake anataka kuwa nani katika aliosomea.

Amesema kuwa suala la ajira nchini zipo za kutosha changamoto ajira ambazo wanazotaka za kukaa ofisini huku wakisahau ujuzi nao ni ajira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here