Home KITAIFA EWURA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALIMBALI KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI.

EWURA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALIMBALI KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI.

Na Leah Choma, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhamasisha matumuzi ya nishati safi ya kupikia ili kuendana na Mkakati wa Kitaifa.

Amesema Mkakati huo umelenga kuhakikisha watanzania wanahamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Hayo yamebainishwa leo Julai, 5 2024 jijini Dar es Salaam kwenye maonesho ya 48 ya Kibiashara kimataifa na Meneja mawasiliano na uhusiano EWURA, Titus Kaguo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wao katika maonesho hayo.

“Tunawahamasisha wawekezaji wawekeze kwenye vituo vya ujazaji wa gesi asilia ambapo utaratibu umesharekebishwa na TBS kwamba kituo cha mafuta kinaweza kuwa kinauza gesi asili kwenye magari,” amesema Kaguo.

Amesema serikali itaendelea kuhamasisha matumizi ya gesi asilia katika vyombo vya moto ikiwemo magari ili kuendeleza matumizi ya nishati safi huku wito ukitolewa kwa wawekezaji kujikita katika uwekezaji wa vituo vya gesi hiyo –CNG.

Amesema EWURA imekusudia kutumia maonesho hayo katika kutoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zinatolewa na mamlaka hiyo.

Aidha amesema kupitia Maonesho hayo imekuwa fursa kukutana na wadau pamoja na wananchi kwa ujumla kutoa elimu kuhusu masuala ya petroli, umeme, gesi asilia pamoja na maji na usafi wa mazingira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here