Home KITAIFA BADO KUNA CHANGAMOTO YA WAZAZI WENYE WATOTO MAHITAJI MAALUM KUWALETA SHULE NA...

BADO KUNA CHANGAMOTO YA WAZAZI WENYE WATOTO MAHITAJI MAALUM KUWALETA SHULE NA CHUONI KUTOKANA NA CHANGAMOTO ZAO.

Na Esther Mnyika, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Baraza la Taifa la Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Tanzania ( NACTIVET), Bernadetta Ndunguru amesema bado kuna changamoto ya wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalumu kutokana na changamoto zao kushindwa kuwaleta shuleni na chuo kupata elimu kwasababu ni haki yao ya msingi.

Hayo ameyabainisha na leo Julai, 5 2024 na Mwenyekiti huyo alipotembelea banda la Mamlaka ya na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) lilopo kwenye maonesho ya 48 ya Kibashara ya Kimataifa.

Amesema kuwa wenye mahitaji maalumu wanapata stadi, ujuzi waweza kujitegemea wao wenyewe.

“Ni kweli kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto ndani wenye mahitaji maalumu hivyo wanapaswa kuto waficha ndani badala yake waweze kuwaleta VETA wajekujifunza ufundi mbalimbali kama tulivyoshudia kwenye mabanda yao wanafanyakazi na waweze kujiajiri,”amesema Ndunguru.

Ndunguru amesema ametembelea mabanda mbalimbali ameona watu wenye ulemavu wanafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kushona nguo na baadhi ya watu wameka oda za nguo zinatoka vizuri.

“Kuna wengine wanatenageneza mabegi ya shule ya kwenda shule na watu wengeni wanaweza kutumia mabegi hayo chuo cha VETA kinasaidia vijana kuweza kujiajiri kupitia mafunzo waliopata,”amesema.

Ameeleza kuwa VETA wanapotoa mafunzo wasiaangaliea watanzania wa kawaida waangalie na wenye mahitaji maalumu kwasababu na wao wana mahitaji muhimu.

Amesema hicho ni kitu cha pekee kinafanywa na VETA wanaona watu wenye mahitaji maalumu wanavyoshughulika na kazi.

Amesema wakipatiwa ujuzi wa kutosha wateweza kujiajiri ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here