Home KITAIFA WAZIRI MKUU AMEZUNGUMZA A WAKAZI WA KIJIJI CHA MMAWA

WAZIRI MKUU AMEZUNGUMZA A WAKAZI WA KIJIJI CHA MMAWA

Lindi

WAZIRI Mkuu na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa leo  Julai 03, 2024 amezungumza na wakazi wa kijiji cha Mmawa kilichopo katika kata ya Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi.

Akizungumza na Wakazi hao Majaliwa amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kufikisha huduma za jamii ikiwemo Afya, maji, Umeme na Elimu katika maeneo yote nchini.

“Kwa mfano katika Wilaya ya Ruangwa na Nachingwea tuna mradi mkubwa wa maji wa shilingi bilioni 119, kwa mradi huu maeneo mengi hapa yatapata huduma ya maji. Rais Dk. Samia pia aliamua kununua mitambo ya kuchimbia visima vya maji lengo ni kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kwenye maeneo yetu,”amesema.

Aidha, Majaliwa amewataka maafisa kilimo nchini kuweka mpango wa kuwahamasisha na kuwasimamia vijana kuingia katika kilimo cha bustani kwenye maeneo ya mabonde yanayofaa kwa kilimo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here