Home KITAIFA TANESCO YAPATA TUZO YA UTOAJI HUDUMA BORA 77

TANESCO YAPATA TUZO YA UTOAJI HUDUMA BORA 77

Na Esther Mnyika, Dar es Salaam

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limepata tuzo ya utoaji huduma bora ambayo imetolewa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (DIT).

Pia limeshukuru wadau kwa kutambua mchango wao katika katika jamii ya utoaji huduma bora kwa wananchi na kupelekea kupata tuzo ya mtoa huduma bora

Akizungumza leo Julai, 3 2024 mara baada ya kupata tuzo hiyo Afisa Masoko TANESCO Makao Makuu, Innocent Lupenza amesema tuzo hiyo kwao imekuwa na maana kubwa jmii imetambua mchango mkubwa unaotolewa na shirika hilo katika kuhudumia umma.

“Pamoja na changamoto ndogo ndogo ambazo tunaenda kuzimaliza tunafurahi kuona mchango wetu umeweza kutambuliwa”,mesema Lupenza.

Amesema tuzo hiyo imeongeza morali kwa wafanyakazi kwa kuendelea kufanya kazi bora na nzuri katika kutoa huduma kwa umma.

“Tunashukuru uongozi kwani unatuwezesha kwa yale yote tunayoyataka ili kurahisisha huduma bora kwa wateja wetu”,amesema.

Lupenza amesema kupitia huduma ya Jisoti ambayo inatolewa na TANESCO inamsaidia mwananchi kuweza kupata huduma zote na kuripoti changamoto yeyote ya umeme pindi inapojitokeza.

“Sasa hivi tunekuja na huduma ya Jisoti ili kumsaidia mteja kupata huduma zetu na kuripoti changamoto ya umeme kwa kutumia simu yake ya mkononi kwa kutumia namba 0748550000,”ameleza.

Aidha ametoa rai kwa wananchi kutembelea banda lao lililopo ndani ya viwanja vya maonesho saba saba ili waweze kupata elimu kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika ukiwemo mradi mkubwa wa bwawa la Mwalimu Nyerere.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here