Mwanza
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Lawrence Tax (Mb) Julai, mosi 2024, ametembelea Shule ya Msingi Nyalikungu iliyopo Halmashauri ya Wilaya Magu, mkoani Mwanza, shule ambayo alisoma akiwa Darasa la Saba.
Mara baada ya kuwasili, Dk. Tax alipokelewa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Betty Ngulla na baadaye alimtembeza Waziri Tax kujionea shuleni hapo kujionea hali ya shule hiyo.
Akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya Kitaaluma ya shulu ya Msingi Nyalikungu, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo alimueleza Waziri Tax changamoto ya upungufu wa madawati ambapo Waziri Stergomena Tax ameahidi kutoa madawati 100 ili kupunguza uhaba uliopo.
Akihitimisha ziara yake, Waziri Tax, alipata wasaa wa kuzungumza na Walimu wa Shule ya Nyalikungu na kuwakumbusha na kuwasisitiza umuhimu wao katika kuwajenga wanafunzi, na ustawi wa jamii bora ya Tanzania.