Dar es Salaam
SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imedhatiti kuja na uwekeza wa utalii wa ikolojia kupitia misitu kwa sababu ya uwepo wa madhari nzuri na yenye kuvutia wageni kuja Tanzania.
Kauli hiyo imetolew leo Julai 2 2024 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk, Hassan Abasi alipotembelea banda la wizara katika maonyesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF).
Amesema uwekezaji wa utalii wa ikolojia utahusisha na ujenzi maeneo ya kupumzikia wageni pindi wanapotembelea vivutio vyetu katika maeneo ya uhifadhi.
“ Pia nimepita katika mabanda yetu na nimeona watu wakivutiwa na uwekezaji mwingine wa asali na nyuki kwani wanataka namna ya kuweakeza katika jambo hilo, suala hilo tunalichukua na tutaangalia namna ya kuwasaidia kupitia mfuko wa nyuki na asali,”amesema.
Amesema tafiti zilizofanywa dunia mwaka huu Tanzania kuongoza Afrika kuwa na wageni wengi wa utalii huku mwaka jana ikiwa nafasi ya pili.
“ Bado tuna fursa nyingi za uwekezaji , takwimu zinaonbesha mwaka jana jumla ya watalii kutoka nje milioni 1.8 walitembelea vivutio vyetu na watalii wa ndani ni milioni 1.9 , jumla ni milioni 3.7 hivyo tunaimani dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassani ya kuwa na watalii milioni tano tutaitimiza Desemba, mwaka huu,” amesema.