Home KITAIFA RAIS DK.SAMIA AMPOKEA RAIS NYUSI

RAIS DK.SAMIA AMPOKEA RAIS NYUSI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mgeni wake Rais wa Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam Julai, 2 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam Julai,2 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Msumbiji MFilipe Jacinto Nyusi wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa kwenye mapokezi Rasmi yaliofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam Julai, 2 2024.

Rais wa Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ikulu Jijini Dar es Salaam Julai, 2 2024.

Rais wa Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam Julai,2 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi Ikulu Jijini Dar es Salaam Julai, 2 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Mgeni wake Rais wa Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam Julai,2 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MSamia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi wakati wakishuhudia utiaji saini Hati ya Makubaliano baina ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania na Taasisi ya Msumbiji ya Uwekezaji na Uwezeshaji Usafirishaji Nje ya Nchi, Ikulu Jijini Dar es Salaam Julai,2 2024. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC, Gilead Teri akitia saini Hati hiyo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa AIPEX Gil Da Conceçao Bires kwa upande wa Msumbiji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi wakati wakishuhudia utiaji saini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika masuala ya Afya baina ya Tanzania na Msumbiji Ikulu Jijini Dar es Salaam Julai,2 2024. Kulia ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akionesha Hati ya Mkataba huo pamoja na Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Msumbiji Manuel José Gonçalves.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusiana na Ziara ya Kiserikali ya Mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi Julai, 2 2024.

Rais wa Msumbiji , Filipe Jacinto Nyusi akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusiana na Ziara yake ya Kiserikali nchini Tanzania Julai, 2 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here