Home KITAIFA MAENDELEO YA MRADI WA JULIUS NYERERE YAVUTA HISIA ZA WENGI SABA SABA

MAENDELEO YA MRADI WA JULIUS NYERERE YAVUTA HISIA ZA WENGI SABA SABA

Dar es Salaam

SHIRIKA la Umeme Tanzania,(TANESCO) linashiriki katika Maonesho ya kimataifa ya biashara ya sabasaba kwa mwaka 2024.Maonesho haya yalianza tarehe 28/6/2024 ambapo wananchi wengi wamevutiwa kutembelea Banda la TANESCO ili kujionea maendeleo ya mkubwa wa kimkakati wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) ambalo limefikia asilimia 98.01 ya ujenzi wake kupitia miwani maalum ya uhalisia pepe (VR).

Akizungumza katika maonesho hayo Julai 1,2024 , Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na uhusiano kwa Umma, Irene Gowelle amesema kuwa TANESCO imejipanga vyema katika ushiriki wake kwenye maonesho hayo ili kuwapa fursa wateja na wananchi kufahamu kazi mbalimbali zinazofanywa na Shirika sambamba na utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya umeme, Matumizi Bora ya vifaa vya Umeme,Huduma za kidigitali ,elimu ya nishati safi ya kupikia na maboresho ya mita za LUKU yanayoendelea nchini.

Aidha amewasihi wananchi na wateja kutembelea Banda la TANESCO na kusema kuwa pamoja na elimu inayotolewa lakini pia TANESCO imejipanga kuwazadiwa wateja wake vitu mbalimbali.

TANESCO inashiriki maonesho ya sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba hadi tarehe 13 Julai 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here