Home KITAIFA DOYO AKATA RUFAA AKIDAI UCHAGUZI, UMEKIUKA KATIBA

DOYO AKATA RUFAA AKIDAI UCHAGUZI, UMEKIUKA KATIBA

Dar es Salaam.

ALIYEKUWA mgombea wa nafasi ya uwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Doyo Hassan Doyo amekata rufaa kwenye kamati ya rufaa ya chama hicho, kupinga uchaguzi uliofanyika baada ya kutoridhika na matokeo.


Mbali na kutoridhika na matokeo Doyo ameituhumu kamati ya uchaguzi pamoja na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Hamad Rashid Mohamed, kwa kukiuka katiba na kanuni za chama hicho.
Juni 29 mwaka huu chama hicho kilifanya uchaguzi mkuu wa nne ambapo baadhi, ya viongozi wamemaliza muda wao wa kipindi cha miaka kumi, kwa mujibu wa katiba akiwemo aliyekuwa mwenyekiti Hamad Rashid Mohamed.


Akizungumza leo Julai,1 2024 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Doyo amesema amekata rufaa kwa mujibu wa kanuni za chama za mwaka 2019 kanuni ndogo ya tatu, inayozungumia haki ya rufaa ambayo itatolewa kwa mgombea tu.


“Sheria hii inamtaka atakayekata rufaa kuwasilisha kusudio ndani ya saa 24, baada ya uchaguzi na baadaye rufaa yenyewe ambayo yote tumeshayafanya,”amesema Doyo.

Amesema sababu ya kukata rufaa ni pamoja mkutano wa uchaguzi kuongozwa na mwenyekiti anayemaliza muda wake Hamad Rashid Mohamed badala ya wajumbe kumchagua mwenyekiti wa muda.
Amesema sababu nyingine ni mwenyekiti wa muda baada ya kupatikana ataendesha shughuli ya kumpata mwenyekiti wa kudumu na baada ya hapo, atamkabidhi miti kwaajili ya uchaguzi wa makamu mwenyekiti Bara na Zanzibar.

“Hapa katiba ilivunjwa mwenyekiti anayemaliza muda wake aliongoza kiao kile kinyume na katiba, na hata alipopatikana hakumkabidhi kiti kuendelea na majukumu yake,”amesema Doyo.

Aidha amesema sababu nyingine ni msimamizi wa kutowapa nafasi wapigakura nafasi kinyume na kifungu n kwa kuwasimamia, na kuwaelekeza nani wakumpigia kura.

“Tunapiga matokeo yote ya uchaguzi pamoja na uendeshaji wake na utangazaji wa matokeo, mambo yote haya yalifanyika mbele ya Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa,”amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here