Home KITAIFA CAG KICHERE AMETOA RAI KWA WANANCHI KUTEMBELEA MAONESHA YA 48 SABA SABA

CAG KICHERE AMETOA RAI KWA WANANCHI KUTEMBELEA MAONESHA YA 48 SABA SABA

Leah Choma@ Lajiji Digital

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Charles kichere ametoa rai kwa wananchi kutembelea maonesho ya 48 ya biashara sabasaba ili waweze kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa katika taasisi za serikali katika kuwahudumia wananchi.

Hayo ameyasema leo Julai 1,2024 wakati alipotembelea maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam.

Amesema wananchi wanapaswa kujitokeza ili waweze kujifunza na kuhudumiwa katika taasisi za Serikali na binafsi ambazo zipo kwenye maonesho hayo.

“Hapa nilipo ni banda la ofisi ya Waziri mkuu kuna taasisi zote zilizo chini ya ofisi hiyo sasa ni muda wa pekee kujitokeza kuja kujifunza na kuhudumiwa hapa na kwenye taasisi nyingine nimepata bahati ya kupita kwenye mabanda tofauti nimeona huduma zinazotolewa kiukweli ni muhimu kwa wananchi kufika hapa,”amesema Kichere.

Aidha ameongeza kuwa uwepo wa banda la kuwezesha wananchi kiuchumi katika ofisi ya waziri mkuu ni fursa kwa wananchi kujua namna wanavyoweza kufikiwa na uwezeshwaji huo unaofanywa na ofisi hiyo.

Akizungumzia maonesho amesema kumefanyika maboresho makubwa kwenye maonesho hayo hivyo ni matarajio yake kuona huduma bora zinatolewa lakini pia wananchi wanajitokeza kwa wingi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here