Dar es salaam
TANZANIA inatarajiwa kupokea Ugeni wa Rais wa Msumbiji Philip Jacinto Nyusi ambaye atawasili kwa ziara yake ya siku nne kuanzia Julai 1hadi 4 ,2024 na ndiye mgeni rasmi atakayefungua maonyesho ya 48 ya biashara ya kimataifa (Saba saba) Julai 3, 2024 baada ya hapo ataelekea Zanzibari.
Akizungumza leo Juni, 30 2024 jijini Dar es Salaam na Waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba amesema Rais huyo anayetarajiwa kuwasili nchini Tanzania wito wa mwaliko maalumu aliotumiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani
Makamba amebainisha kuwa, Rais Nyusi atawasili nchini hiyo moja ya mashirikiano mazuri yaliyodumu na ni ya kihistoria ambapo ukiangalia kuna raia wa Msumbiji wapo Tanzania wakifanya shughuli zao za kiuchumi na watu wa nchi kwetu wapo kwao hivyo siyo jambo la kushangaza
Amefafanua ziara hiyo itaanzia pale Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Julai 1 atapokelewa na Viongozi wa mbalimbali na Julai 2 atakutana na Rais Samia Ikulu ambapo watafanya mazungumzo ya faragha watajadili mambo mengi ikiwemo na ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili ili kuimarisha mahusiano yao.
“Rais Philip Nyusi anakuja nchini kwetu kwa ziara ya siku nne ambapo atawasili Julai 1,2023 na atapokelewa uwanja wa ndege wa kimataifa na viongozi mbalimbali wa serikali lakini tarehe 2 atapokelewa rasmi na mwenyeji wake ikulu jijini Dar es Salaam Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na kufanya mazungumzo ya faragha wawili hao,”amesema Makamba.
Amesema pia katika ziara hiyo watasaini mikataba ya ushirikiano katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya Elimu , madini pamoja na mashirika ya habari lengo ni kuongeza mahusiano mazuri hasa katika kuimarisha ulinzi na usalama baina ya nchi hizo mbili hususani maeneo ya mpakani
Aidha amesema kuwa biashara katika nchi hizo bado sio mzuri kutokana biashara zinafanyika mpakani hazirikodiwi ambapo Tanzania ndio imekua ikipeleka bidhaa nyingi zaidi Msumbiji kuliko nchi hiyo kuleta huku.
“Tanzania tumekuwa tukiuza zaidi biashara nchini mwao ambapo hadi mwaka 2022 tuliuza dolla za kimarekani mill 57 lakini wao wameuza dolla za kimarekani mill 4.8, Lakini kwa mwaka 2023 Tanzania ilishuka hadi dolla za kimarekani mill 20, “amesema Makamba.
Pia kupitia ziara hiyo Rais Nyusi atawaaga watanzania kwani muda wake wa kukaa madarakani umeisha, hivyo ziara hiyo itakua ndio ya mwisho nchini Tanzania, kuja akiwa madarakani lakini tayari Rais kupitia chama cha FRELIMO Daniel Francisco Chapo alishawahi kuja kutambulishwa Tanzania hivyo akikabidhi kijiti atakuwa ameziacha nchi hizo na historia ya ukaribu ukiimarik.
Aidha Nchi ya Msumbiji miaka miwili iliyopita ilikua inakabiliwa na changamoto ya ulinzi na usalama hivyo kutokana na ukaribu uliopo wanajeshi kutoka Tanzaia chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC walipelekwa kwenda kusaidia kuimarisha hali ya Ulinzi na usalama hivyo kupitia ziara hiyo ni chachu ya kuimarisha mahusiano mazuri yaliopo baina Mataifa hayo mawili.