Home KITAIFA WEZESHENI WATU VYA KUTOSHA WATUMIE GESI KWENYE MAGARI; YASEMA KAMATI YA BUNGE

WEZESHENI WATU VYA KUTOSHA WATUMIE GESI KWENYE MAGARI; YASEMA KAMATI YA BUNGE

πŸ“Œ Yaitaka TPDC kuongeza vituo vya kujaza gesi

πŸ“Œ Yaitaka pia kuongeza karakana za kuweka mifumo ya CNG

πŸ“Œ Wizara ya Nishati yaahidi kuendelea kuiwezesha TPDC kutekeleza majukumu yake

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imelielekeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC) kuongeza uwezeshaji kwa wananchi ili waweze kuhamasika kutumia mfumo wa gesi kwenye magari yao kwani una gharama nafuu na utaokoa fedha za kigeni zinazotumiwa na Serikali kuagiza mafuta nje ya nchi.

Mwenyekiti hiyo, Dk. Mathayo David Mathayo amesema hayo wakati wa semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kupitia TPDC ya kuwaelimisha Wabunge juu ya mkakati wa TPDC kwenye utekelezaji wa miradi yake ya kimkakati kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025.

β€˜β€™ Wananchi wanahitaji sana huduma ya gesi kwenye magari yao lakini upatikanaji wa vituo vya kujaza gesi ndio hofu yangu, nashauri mjipange kuhakikisha kila Mkoa angalau unakuwa na vituo ili kusogeza huduma karibu na wananchi,’’amesema Dk. Mathayo.

Ameeleza kuwa, Tanzania inayo hazina kubwa ya gesi hivyo ni vema kutumia fursa hiyo kwa kutoa kipaumbele kwenye utekelezaji wa miradi hiyo na kuongeza kuwa TPDC ione umuhinu wa kusogeza karakana za kuweka mifumo ya CNG kwenye magari kwenye maeneo mengine, badala ya kutegemea Dar es salaam pekee jambo ambapo ni usumbufu na gharama kuifuata huduma huko.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk. James Mataragio amesema, Wizara ya Nishati itaendelea kuiwezesha TPDC kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha utekelezaji wa miradi hii inakuwa na tija na kukamilika kwa wakati na ndio maana wamehusisha sekta binafsi kushiriki kwenye ujenzi wa vituo vya CNG na kuwezesha karakana za kuweka mifumo ya CNG kwenye Magari .

Katika mwaka wa fedha wa 2024/2025 TPDC inejipanga kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya utafutaji wa gesi na uendelezaji wa mafuta, miradi ya usafirishaji na usambazaji wa gesi,miradi ya kutekeleza mkakati wa Nishati safi ya kupikia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here