Home AFYA WANANCHI SERENGETI WAPAZA SAUTI KUMSHUKURU RAIS SAMIA UJIO WA MADAKTARI BINGWA

WANANCHI SERENGETI WAPAZA SAUTI KUMSHUKURU RAIS SAMIA UJIO WA MADAKTARI BINGWA

Na Shomari Binda-Serengeti

WANANCHI wilayani Serengeti mkoani Mara wamepaza sauti ya kumshukuru Rais Dk.Samia kwa kuapelekea madaktari bingwa wa kuwatibu.

Wakizungumza kwenye hospital ya Wilaya ya Serengeti leo juni 28 baada ya kupata huduma za madaktari hao ikiwa ni siku ya mwisho ya utoaji huduma wamesema jambo walilofanyiwa la kuokoa maisha yao limewapa faraja.

Wamesema Rais Dk.Samia ameonyesha upendo wa hali ya juu maana suala la afya ni jambo la msingi ili kuendelea kushiriki shughuli za kijamij na kiuchumi.

Mmoja wa wananchi waliopata matibabu ya madaktari hao aliyejitambulisha kwa jina la Mseti Warioba aliyekuwa akisumbuliwa na uvimbe kwenye mguu ameshukuru baada ya kufanyiwa upasuaji.

Amesema ameangaika kwa muda mrefu na amekuwa akishindwa hata kuinama lakini baada ya upasuaji sasa anaweza kuinama.

” Tunamshukuru sana Rais Dk.Samia kwa ujio wa madaktari hawa ambao wamekuja kutusaidia na kuepusha gharama kubwa za fedha kuwafuata walipo,”amesema.

Mariam Matiku ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo la uzazi amesema amekutana na daktari wa tatizo lake na kupata vipimo,matibabu na ushauri na amehudumiwa vizuri na kushukuru ujio wao.

Daktari Bingwa wa mMgonjwa ya Wanawake na Uzazi Dk.Godwin Silas Macheku ambaye ni kiongozi wa timu ya madaktari wa Rais Samia waliopo Serengeti amesema muitikio umekuwa mkubwa wa wananchi kufika na kupatiwa huduma.

Amesema kwa siku ya nne kati ya siku tano za huduma wamewahudumia wananchi zaidi ya 400 wakiwemo wa upasuaji na magonjwa mengine ambayo hayahitaji upasuaji.

Kwa upande wake Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti, Johansen Bakuba kwa niaba ya mganga mfawidhi wa Hospital hiyo amesema licha ya madaktari hao kutibu wananchi lakini waewaongezea uwezo watumishi wa hospital hiyo wakiwemo watumishi wa hospital ya Nyerere DDH wanaoshiri nao kwenye huduma ya madaktari hao.

Amesema wanamshukuru Rais Dk.Samia kwa program ya madaktari hao ambayo imekuwa msaada kwa wananchi na watumishi wa hospital.

Aidha Bakuba ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa ya kukutana na madaktari bingwa kila wanaposikia wamefika hospitalini hapo ili kupata huduma za kibingwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here