Home BIASHARA TRADE MARK AFRIKA KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI NCHINI

TRADE MARK AFRIKA KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI NCHINI

Na Saidina Msangi,Dodoma.

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Amina Khamis Shaaban, ameongoza Mkutano wa 47 wa Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee -NOC) inayosimamia utekelezaji wa miradi ya kuwezesha na kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa ufadhili wa TradeMark Africa (TMA), kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Natu El- maamry Mwamba.

Mkutano huo umeidhinisha bajeti ya mwaka 2024/2025 kiasi cha dola za Marekani milion 7.1 ambayo itatekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuongeza ufanisi wa biashara nchini na ukanda kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo kwa vijana na wanawake katika kufanya biashara hususan katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

Mkutano huo pia umepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa miradi ya TMA kwa mwaka 2023/2024 ambapo ilibainishwa kuwa kwa kipindi cha Julai 2023 – Juni 2024, miongoni mwa mafanikio ni kukamilika kwa Sera ya Biashara (National trade policy) ambayo itazinduliwa Julai, 11 2024.

Mafanikio mengine ni kukamilika na kuzinduliwa kwa Mfumo wa Kieletronic wa Uwekezaji (Tanzania Investement Single Window System) ambao unawezesha wawekezaji kuomba vibali vya uwekezaji kwa njia ya mtandao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here