Home KITAIFA MAHIMBALI ASISITIZA GST KUWAFIKIA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI NCHINI

MAHIMBALI ASISITIZA GST KUWAFIKIA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI NCHINI

Dodoma

KATIBU Mkuu Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali ameiagiza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kupanua wigo wa huduma zake ili kuwafikia wachimbaji wadogo wa madini na kuongeza juhudi za kujitangaza.

Mahimbali ametoa maagizo hayo leo Juni 27, 2024 alipotembelea Banda la GST katika Wiki ya Madini iliyoratibiwa na Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) yanayofanyika katika Viwanja vya Jakaya Convention Centre (JKCC) jijini Dodoma.

Amesema, GST ishirikiane na Tume ya Madini pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika kuhakikisha wanawafikia wachimbaji wadogo kwenye maeneo yao na kuwafanyia tafiti ili waweze kuchimba kwa tija na kuongeza faida kwa Wachimbaji hao na kuleta manufaa kwa Taifa.

Aidha, Mahimbali ameitaka Taasisi hiyo kuendelea kujitangaza ili iweze kufahamika Duniani kote kwa kutoa taarifa za uhakika katika utafiti wa madini pamoja na tafiti za uchenjuaji wa madini.

Pamoja na mambo mengine, Mahimbali ametoa siku 100 kwa uongozi wa GST kuhakikisha wanafanya mabadiliko ili kuifanya kuwa taasisi shindani duniani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here