Home KITAIFA KAMATI YA BUNGE YA PAC YAPIGWA MSASA

KAMATI YA BUNGE YA PAC YAPIGWA MSASA

📌 Ni kuhusu miradi inayotekelezwa na wizara kupitia TPDC

📌 DKt Biteko afungua rasmi, aishukuru PAC kwa mchango wao sekta ya Nishati

📌 Waitaka TPDC kuwekeza kwa kutumia fedha za ndani na sio kutegemea wafadhili pekee

Na Mwandishi wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko ameipongeza kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kwa kusimamia na kushauri vema mashirika yanayotekeleza miradi mbalimbali ya serikali, kwani wamekuwa wakitoa mchango mkubwa kwenye mafanikio ya miradi hiyo.

Dk. Biteko ameyasema hayo wakati akifungua semina ya kamati ya Bunge ya PAC iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) wakati wakiwasilisha mpango wa bajeti ya miradi ya maendeleo itakayotekelezwa na TPDC kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Dk. Biteko amesema kupitia bajeti hiyo TPDC itatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo uchorongaji wa visima vya kutafuta gesi eneo la Mnazi Bay pamoja na kumtafuta mbia kwa ajili ya kushirikiana nae kwenye kazi hiyo pamoja na kukamilisha tafsiri ya taarifa za mitetemo kwenye kitalu cha Eyasi-wembere.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Kamati ya PAC Japhet Hassunga ameitaka TPDC kuangalia uwezekano wa kuwekeza mtaji wa kutosha kwenye miradi ya gesi badala ya kutegemea wafadhili pekee na kutolea mfano nchi ya Misri ambapo uwekezaji wa Suez Canal ulifanikishwa na wananchi wa Misri kwa kutoa fedha za uwekezaji na kufanikiwa kwenye mradi huo,hivyo ni vema kuiga kutoka kwa wenzetu

Amesema nchi nyingi duniani zenye utajiri wa gesi na mafuta zimeendelea sana na kwa kuwa Tanzania inayo gesi ya kutosha, hatupaswi kuendelea kuwa maskini hivyo ameitaka TPDC kuwekeza kwenye uchorongaji na taarifa za upatikanaji wa rasilimali hizo.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dk. James Mataragio ameihakikishia Kamati kuwa Wizara itaendelea kusimamia miradi ya kimkakati inayotekelezwa na taasisi zake hususani ile ya kusambaza gesi kwani iko kwenye mkakati wa Serikali na kwenye dira ya maendeleo ya Serikali.

Ameitaka TPDC kuishirikisha Sekta binafsi kwenye utekelezaji wa fmiradi yake kwani TPDC pekee haiwezi kufanikisha na kuahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here