Home AFYA UONGOZI WA MUHIMBILI-MLOGANZILA WAKUTANA NA CHUO KIKUU CHA YONSEI

UONGOZI WA MUHIMBILI-MLOGANZILA WAKUTANA NA CHUO KIKUU CHA YONSEI

Dar es Salaam

UONGOZI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili -Mloganzila umekutana na kufanya mazungumzo na jopo la wataalam kutoka Shule ya Uzamili ya Afya ya Jamii Chuo Kikuu cha Yonsei cha nchini Korea Kusini.

Mazungumzo hayo yamelenga katika kubadilishana uzoefu na kuangalia fursa ambazo pande zote mbili zinaweza kushirikiana ili kuendelea kuimarisha huduma za afya hapa nchini.

Akizungumza na wataalam hao, Naibu Mkurugenzi Mtendaji, MNH-Mloganzila Dk. Julieth Magandi amesema huduma za hospitali ya Mloganzila zimeendelea kuwa bora na kuifanya jamii kuvutiwa na huduma zinazotelewa ambapo kwa sasa wanahudumia kati ya wagonjwa 900 hadi 1000 kwa siku.

“Kutokana na ubora wa huduma, vifaa tiba, mazingira na wataalam waliopo, hospitali hii imeendelea kuwa kimbilio kwa Watanzania na watu kutoka nje ya chi kupata matibabu, hivyo na sisi kama wataalam tunaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyowekwa na serikali,’’ ameeleza Dk. Magandi.

Aidha, ameshauri jopo hilo kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya tafiti na machapisho kwa kuweka nguvu katika namna ya kuzuia maambukizi ya magonjwa, kuendelea kuwajengea uwezo wataalam hususani wa vifaa tib

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here