Home KITAIFA SERIKALI YASITISHA ZOEZI LA UKAGUZI WA RISITI ZA EFD KARIAKOO

SERIKALI YASITISHA ZOEZI LA UKAGUZI WA RISITI ZA EFD KARIAKOO

Dodoma

SERIKALI imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, JijiniĀ  Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariokoo.

Hayo yamesemwa kwa niaba ya Serikali, jijini Dodoma, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba na kuhudhiriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here