Home KITAIFA MOTO WATEKETEZA MAKAZI YA KAYA 43 KISIWA CHA RUKUBA MUSOMA VIJIJINI

MOTO WATEKETEZA MAKAZI YA KAYA 43 KISIWA CHA RUKUBA MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

JUMLA ya makazi ya kaya 43 kwenye kisiwa cha Rukuba kilichopo Musoma vijijini zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.

Moto huo umedaiwa kuharibu mali mbalimbali za wananchi ikiwemo vyakula na kuomba msaada wa kibinadamu kutoka kwa serikali na jamii.

Kwa mujibu wa taarifa toka ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo imedai kaya hizo zimepatwa na maafa makubwa ya moto kuteketeza makazi na mali zao.

Taarifa hiyo imesema viongozi na wakazi wa kisiwani hapo wanaendelea kusomba mabaki ya vyombo vya waathirika na kuweka utaratibu wa kupata makazi ya muda kwa baadhi ya kaya zilizoathirika.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kutokana na moto huo anatoa pole nyingi sana kwa waathirika wa janga hilo la moto na anaendelea kuwasiliana wa viongozi wa Kisiwa cha Rukuba.

” Nawapa pole sana wote walioathirika na janga hili la moto kwenye kisiwa chetu cha Rukuba tunashukuru Mungu hakuna taarifa ya kifo na tunaendelea kufanya mawasiliano zaidi.

” Nawaomba wote walioathirika kuwa wastahimilivu wakati tukiendelea na jitihada za msaada zaidi”,amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here