Home KITAIFA DK. MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA TAASISI YA BIG WIN

DK. MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA TAASISI YA BIG WIN

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Taasisi ya Big Philanthropy ya Uingereza kushirikiana na Serikali kwa mpango wa lishe mashuleni katika kupunguza utoro na kuongeza ufaulu.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Big Win Philanthropy, Dk. Kesete Admasu na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar Juni, 25 2024.

Aidha Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Dk. Admasu ameleeza kuwa wako tayari kushirikiana na Serikali katika fursa za kuwajengea uwezo watendaji wa Serikali na viongozi pamoja na ushirikiano wa sekta mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here