-Asema falsafa ya Dk. Samia ni kutatua migogoro kwa kukaa mezani pamoja
-Asisitiza kamwe migogoro haiwezi kusuluhishwa kwa mashinikizo
Dar es Salaam
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila leo Juni 24,2024 amefika eneo la Kariakoo maarufu kwa shughuli mbalimbali za kibiashara jijini humo kwa lengo la kujionea hali halisi kufuatia mgomo wa wafanyabiashara ambapo amejionea baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa na mengine yamefunguliwa.
RC Chalamila amesema eneo hilo lina amani na usalama wa kutosha ambapo amewataka wafanyabiashara waliofungua maduka kuendelea kufanya biashara kwa uhuru kamwe asitokee mtu hata mmoja kushinikiza waliofungua wafunge maduka yao.
Aidha RC Chalamila amesema Falsafa ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kutatua migogoro kwa kukaa mezani pamoja ambapo akasema hata sasa ninavyoongea viongozi wa wafanyabiashara tayari wako Dodoma kwa lengo la kupata Suluhu za changamoto za wafanyabiashara hivyo kufunga maduka ni kukosa uvumilivu alisisiza RC Chalamila.
Vilevile RC Chalamila ametoa rai kwa wafanyabiashara wa Kariakoo kutatua migogoro kwa kukaa mezani pamoja na Serikali kamwe migogoro haiwezi kutatuliwa kwa mashinikizo ni vema kuilinda Dar es Salaam kwa nguvu zote kwani amani ikitoweka hakuna mkoa mwingine ambao wataweza kufanya biashara
RC Chalamila amewahakishia wafanyabiashara wote wa Kariakoo waliofungua na waliofunga kuwa eneo hilo ni salama ulinzi ni wakutosha wanaofanya biashara waendelee kufanya bishara zao kwa uhuru.