Na Shomari Binda-Musoma
MADAKTARI bingwa wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan wataanza kutoa huduma za matibabu ya kibingwa kwenye hospital ya manispaa ya Musoma kesho 24 hadi 28 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo juni 23,Mganga Mfawidhi wa Hospital hiyo Dk.Emanuel Shani amesema maandalizi yote ya madaktari hao kuanza kuwahudumia wananchi yamekamilika.
Amesema wananchi zaidi ya 200 hadi jana juni 23 walikuwa wamekwisha kujiandikisha tayari kwa kupokea huduma hizo za kibingwa kutika kwa madaktari bingwa wa Rais Dk.Samia
Dk. Shani amesema shughuli ya uandikishaji inaendelea kufanyika hospitalini hapo ambapo matibabu yatazingatia uandikishaji uliofanyika.
Amesema fursa ya madaktari bingwa hao wa Rais Dk.Samia inakuja kwenye hospital ya manispaa ya Musoma hivyo wananchi wenye matatizo mbalimbali wanapaswa kuitumia.
Mganga Mfawidhi huyo amesema madaktari hao watatibu magonjwa ya kina mama,magonjwa ya watoto,upaduaji wa mfumo wa mfumo wa mkojo,magonjwa ya ndani,usingizi na ganzi,macho,mifupa pamoja na mionzi radioloji.
” Tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa madaktari bingwa kutufikia kwenye hospital yetu ya manispaa ya Musoma.
” Maandalizi yote ya kuwapokea madaktari kabla ya kuanza kutolewa kwa huduma kesho juni 24 yamekamilika na wananchi wamejitokeza kujiandikisha,”amesema.
Amesema wanamshukuru pia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya uboreshaji wa hospital ya manispaa ya Musoma.
Dk.Shani amesema uboreshaji huo umeendana na wodi za ” VIP” na ujenzi wa majengo mapya ya wagonjwa wa dharura pamoja na kinywa na meno.
Aidha Dk.Shani wameishukuru Ofisi ya MSD kanda iliyopo Mwanza kwa kuifikishia hospital dawa na vifaa tiba kwa wakati na kuwezesha wananchi kupata huduma stahiki.
Baadhi ya wananchi waliofika hospitalini hapo kwaajili ya kujiandikisha wamemshukuru Rais Dk.Samia kwa huruma yake kwa kuwaletea madaktari bingwa.
Wamesema wataitumia fursa hiyo kwa kuwa ni gharama kuwafuata kwenye hospital kubwa kwaajili ya kupata matibabu.