Home KITAIFA TANZANIA YASISITIZA MATUMIZI YA KISWAHILI EAC

TANZANIA YASISITIZA MATUMIZI YA KISWAHILI EAC

Dar es Salaam

SERIKALI ya Tanzania imeendelea kutoa msisitizo wa matumizi ya lugha ya Kiswahili katika shughuli mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo mikutano na warsha.

Msisitizo huo umetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo M Dk. Damas Ndumbaro katika mkutano wa 19 wa Baraza la Mawaziri wa Kisekta wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo leo Juni 22, 2024 Jijini Dar Es Salaam.

“Katika mkutano huu sisi Jamhuri ya muungano wa Tanzania tumesisitiza matumizi ya lugha yetu pendwa ya Kiswahili iweze kutumika katika vikao vya jumuiya ya Afrika Mashariki na hatimaye tuweze kuikuza tuipeleke Umoja wa Mataifa,”amesema Dk. Ndumbaro

Kwa upande wake Waziri wa Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Torati za Taifa wa Kenya MAisha Jumwa amesema amewakaribisha wanajumuiya hiyo katika maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani Julai 7, 2024 ambayo yatafanyika nchini humo na maandalizi yanaendelea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here