Dar es Salaam
RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania na Guinea Bissau zina mambo mengi ya kushirikiana katika kukuza uchumi wa buluu na kilimo cha korosho zao hilo ambalo linalimwa katika nchi zote mbili.
Akizungumza leo Juni 22 Ikulu Jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari baada ya kumaliza mazungumzo baina ya serikali ya Tanzania na Guinea Bissau Rais Dk. Samia amesema nchi zote mbili zina eneo kubwa la bahari hivyo wamepanga kushirikiana katika kukuza uchumi wa buluu.
Amesema nchi hizo zitashirikiana katika kukuza maeneo huru ya uwekezaji EPZA ambapo pia Rais wa Guinea Bissau aliyopo nchini atafanya ziara ya kukagua maeneo hayo nam kutembelea Reli ya Kisasa (SGR) inakwenda Burundi, D.RC na maeneo mengine ya Afrika.
“Nchi hizi zimepanga kukuza biasha baina yao hasa zao la korosho na hasa kuongeza tafiti za kukuza uzalishaji wa zao hili na kuongeza thamani,”amesema Dk. Samia.
Amesema ziara hiyo ni msingi wa kuimarisha uhusiano wa kudumu ulioasisiwa na waasisi wa Mataifa hayo na viongozi hao walikuwa na dhamira moja ya umajumui na kupinga ukoloni wakati huo.
Ameeleza kuwa itakumbuka Tanzania ilikuwa Mwenyekiti wa nchi wanachama wa ukombozi ambao baadaye ukabadilika na kuwa Umoja wa Afrika na ziara ya Rais huyo imeleta fursa ya kufanya mazungumzo na kujadili yaliyoasisiwa na waasisi wa Mataifa hayo.
Rais Dk.Samia ametaja miongoni mwa mambo waliyoyazungumza ni katika masuala ya kiuchumi, kikanda na ukuzaji Amani na usalama,Biashara na Uwekezaji na ushirikiano katika sekta ya kilimo cha korosho, afya na elimu, ulinzi na usalama na masuala ya kimataifa na Kupamba dawa za kulevya.
“Bara lipo katika mbio za kuhakikisha biashara inafunguka Afrika kutakapochochea ongezeko la viwanda.Tumekaa pamoja kuhakikisha eneo hilo linatumika ipasavyo,”amesema.
Ameongeza kuwa wamekubaliana kushirikiana na nchi nyingine za Afrika kuhakikisha bei za bidhaa za kilimo zinapata bei nzuri kwa kutengeneza sauti moja.
Aidha Dk. Samia amesema nchi hizo mbili zina eneo kubwa la mwambao wa Pwani na zote zipo katika nafasi nzuri ya kufanya biashara na zinapakana na nchi zisizo na mwambao.Utalii, uvuvi hasa wa fukwe.
Amesema uwekezaji na biashara ni eneo walilokaa kujadiliana na wamesaini mkataba wa kuanza mazungumzo kwenye eneo hilo.
Akizungumza Rais wa Guinea Bissau, Umaro Sissoco Embaló amesmea nimefurahi kuwa na ziara Tanzania na naleta salamu za dhati za watu wa Guinea.
Ameeleza kuwa mataifa hayo yameshirikiana katika kuondoa ukoloni na ubaguzi wa rangi na kazi hiyo ilifanyika katika Jiji la Dar es Salaam.
“Nipo hapa kutoa heshima kwa Mwalimu Julius Nyerere ambaye mwaka 1979 alitembelea nchini kwetu na watu wetu walimpokea na kumpa medali ya heshima,” amesema Rais Embalò.
Ameeleza kuwa ndiye aliyekuwa Rais wa kwanza kutoka nje ya Guinea Bissau kupokea medali hiyo na ilitokea kwa sababu ya kuleta mchango wake.
Amesema mataifa ya afrika yakishirikiana Yana uwezo wa kuandaa mustakabali wa dunia, kwa kuwa ina rasilimali za kutosha na viongozi bora.
Amesema Tanzania na Guinea zikifanyakazi pamoja zinaweza kuchangia agenda ya Afrika ya mwaka 1963 kuwa na amani ya kudumu na ustahimilivu wa kisiasa.
Amesema kwa umoja huo wataweza kuwa na kazi nzuri na sekta binafsi imekaribishwa kwenda Guinea Bissau ili wakanufaike kibiashara.
Ameeleza kuwa nchi hiyo inaweza kuwa lango muhimu wa kuingia katika mataifa ya magharibi.
“Ni muhimu kubadilisha mahusiano yawe imara zaidi kwani Guinea Bissau hawawezi kusahau kuhusu Tanzania na wamekuwa wakufunzwa kuhusu Mwalimu Nyerere shuleni,” amesema.
Amesema wapo tayari kuwasaidia wakiwahitaji na ndiyo maana yuko nchini kwa sasa na atakaporejea hatakwamisha mkataba uliosainiwa.
Ameongeza kuwa atawaleta wanafunzi wa Kiswahili kuja kujifunza na kwamba alisema akijifunza kishwahili kwa kuwakitawafunza na ni lugha ya Afrika.
Aidha amemwalika Rais Dk. Samia kwenda nchini Guinea Bissau na ataangalia muda mwafaka wa kwenda nchini humo.