Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimpokea Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló leo Juni, 22 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Embaló yuko nchini kwa ziara ya kikazi.
Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam Juni,22 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.