Home KITAIFA NAPE AMEWATAKA MAAFISA HABARI UJUZI WALIOPATA KUBORESHA UTENDAJI WAO

NAPE AMEWATAKA MAAFISA HABARI UJUZI WALIOPATA KUBORESHA UTENDAJI WAO

Dar es Salaam

WAZIRI wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewataka Maafisa Habari watumie ujuzi waliopata kuboresha utendaji wao na ujuzi watauona kwenye utendaji.

Hayo ameyasema Juni, 21 jijini Dar es Salaa Nnauye wakati akifungua Kikao kazi cha Maafisa Habari wa Serikali kilichofanyika siku mbili amesema kikao hicho wameweza kufahamiana kubadilishana ujuzi na uzoefu.

Amesema pamoja na kazi ya kuhabarisha umma yanayoendelea kwenye serikali na umma wakifanya hivyo wametimiza wajibu wao.

“Utendaji kazi uwe na ubora hasa kwenye zama hizi za uwazi wa Sayansi ya teknolojia jamii iwe na taarifa sahihi kuhusu serikali wawe na imani na huduma zetu, kufanya taasisi ibadiliike ili tueleze habari njema kwa taasisi zetu tufanye kazi,”amesema Nnauye.

Akizungumzia kuhusu Maafisa Habari kuwa na vifaa vya kisasa Nnauye amesema wahitaji kuwa na vifaa vya kufanya kazi viendane Sayansi na Teknolojia na vifaa vya kutosha kwaajili yao na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa IdarayaHabariMaelezo kusimamia hilo.

Amesema hawawezi kuwa na matokeo mazuri bila kuwa na vifaa vizuri fanyeni tathimini.

Ameongeza kuwa pamoja na hayo Maafisa Habari kuwa na hadhi kwenye taasisi zao kuanzia Halmashauri, Taasisi na Wizara hilo limebadilika hadi kuelekea kwenye Uchaguzi kuwe na mabadiliko.

Aidha amemuagiza Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo kuweka utaratibu wa mafunzo ili kuwatengeneza ujuzi na kubadilishana uzoefu kwa sababu Rais Dk.samia Suluhu Hassan anawaamini wataenda kutengeneza picha nzuri ya nchi.

Awali Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Thobias Makoba wakati akisoma maadhimio manne ya kikao hicho baadhi ya pamoja na maafisa habari waongeze kasi ya utekelezaji wa miradi kwa wananchi kuzingatia weledi wa waandishi wa habari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here