Home KITAIFA WAZIRI MKUU AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC

Dar es Salaam

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa Leo Juni 21, 2024 amekutana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Katibu wa Kamati ya CPC Jimbo la Shanxi nchini China.

Katika mazungumzo yao ambayo yamefanyika kwenye Ofisi ndogo za Waziri Mkuu, Magogoni Jijini Dar es Salaam, Majaliwa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa amesema kuwa Tanzania itaendeleza mahusiano na China kwenye maeneo ya Siasa, Kijami na Kiuchumi.

Kwa upande wa Chama cha Mapinduzi kiliwakilishwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (MCC) , Rabia Abdalla Hamid.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here