Home KIMATAIFA CCM CHINI YA MWENYEKITI DK. SAMIA IMEENDELEA KUTUAMINI VIJANA, TUCHAPE KAZI TUSIMUANGUSHE...

CCM CHINI YA MWENYEKITI DK. SAMIA IMEENDELEA KUTUAMINI VIJANA, TUCHAPE KAZI TUSIMUANGUSHE – CDE. JOKATE

Iringa

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Komredi. Jokate Mwegelo, amewataka vijana wote wanaoaminiwa na kupewa nafasi za uongozi ndani ya chama au serikali kufanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu wa hali ya juu kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.

Komredii Jokate ameyasema hayo wakat akizungumza kwenye kikao na viongozi wa Chama na Jumuiya ya UVCCM Mkoa wa Iringa mara baada ya kuwasili na kupokea taarifa ya kazi ya UVCCM mkoani humo.

“Yatupasa wakati wote kutoa shukrani kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachoongozwa na Mwenyekiti na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutuamini vijana hususani vijana wa kike na kutuamini katika kutupa nafasi za uongozi ndani ya chama na serikali yetu hivyo ni wajibu na ulazima kufanya kazi kwa bidii na ubunifu kwa manufaa ya chama, serikali na Taifa kwa ujumla,”amesema.

Akiendelea kuzungumza na viongozi hao, Komredi Jokate amesisitiza juu ya Ushirikano katika kufanya kazi.

“Kikubwa kwetu ni ushirikiano wa kutosha na kufanya kazi kubwa kulingana na wajibu wetu katika kuhakikisha vijana wanapata fursa mbalimbali hususani kuwainua kiuchumi, kuendelea kuwasemea vema viongozi wetu wa chama na serikali na kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola,”amesema.

Aidha, Komredi Jokate amesema lengo kubwa la kuwasili mkoani Iringa ni mpango mkakati wa kuinua kituo cha Ihemi kuwa chachu na fursa zaidi kwa vijana.

“Tumekuja hapa kuangalia fursa za kuendeleza kituo chetu cha Ihemi na hivi karibuni tutakuwa na mafunzo kwa viongozi wetu wa wilaya nchi nzima,”amesema.

“Tunataka kuimarisha kituo cha Ihemi na kwa namna tulivyojipanga tuna hakika tutaweza kufikia adhma hiyo.

“Niwasihi vijana wenzangu wa CCM , chama chetu kina namna na utartibu wake wa kuwasilisha majambo yetu na changamoto zetu hata za baina yetu ya sisi kwa sisi kupitia vikao na si kutumia njia zingine ambazo ni sawa na kuwa faida wapinzani kupata la kusemea, tuwe wazalendo, tupende chama na nchi yetu na tuwe na utulivu,” ameongeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here