Home KITAIFA BRELA YATAKA WANANCHI KUSAJILI MAJINA YA BIASHARA ZAO

BRELA YATAKA WANANCHI KUSAJILI MAJINA YA BIASHARA ZAO

Morogoro

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umewahimiza Wananchi kusajili majina ya biashara zao.

Hayo yabenainishwa Juni 19, 2024 mkoani Morogoro na Mkuu wa Sehemu ya Kampuni kutoka Kurugenzi ya Kampuni na Majina ya Biashara wa BRELA Lameck Nyange akiwasilisha mada kuhusu Majina ya Biashara (Sheria na huduma baada ya Sajili) katika siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi wa habari wanaoripoti habari za biashara kutoka mkoani Dar es Salaam.

Samson amebainisha kuwa moja ya faida ya kufanya usajili wa majini ya biashara ni kusaidia kumlinda mwanzilishi wa jina hilo ili lisijekuchukuliwa na kusajiliwa na mtu mwingine na hivyo yeye kupoteza umiliki wake.

“Usajili wa majina ya biashara ni muhimu sana kwa ajili ya kumlinda mmiliki wa jina husika. Hii itasaidia kuzuia BRELA kulisajili kwa mtu mweingine. Kwa hiyo kila mfanyabiashara ni muhimu kusajili majina ya biashara zao,” amesema Samson.

Amebainisha kuwa faida nyingine ya kusajili jina la biashara, ni kuwasaidia BRELA kutorudua kulisajili tena jina hilo.

Akifafanua kuhusu majina ambayo hayawezi kusajiliwa, ameyataja baadhi kuwa ni pamoja na majina ambayo kwa namna moja ama nyingine ni matusi, majina ambayo yanataja jina ama chombo cha Serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here