Home KITAIFA BODI YA TANESCO YAFURAHISHWA NA KUPONGEZA MAENDELEO YA UJENZI MRADI WA JULIUS...

BODI YA TANESCO YAFURAHISHWA NA KUPONGEZA MAENDELEO YA UJENZI MRADI WA JULIUS NYERERE

Na Charles Kombe, Rufiji

BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imefurahishwa na kupongeza wasimamizi wa mradi juu ya hatua za ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa bwawa la Julius Nyerere (JNHPP).

Hayo yamebainishwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Zuhura Bundala walipokua kwenye ziara ya wajumbe wa bodi hiyo kutembelea mradi huo Juni 19 wakiambatana na kaimu Mkurugenzi wa Shirika upande wa uzalishaji Mhandisi Abubakar Issa.

“Niwaambie watanzania kujivunia Serikali yao inayopenda nchi na wananchi maana huu mradi ni mkubwa. Naipongeza TANESCO kwa kuendelea kusimamia ujenzi wa mradi huu,” amesema Bundala.

Ameongeza kuwa “taarifa tuliyopewa na wataalamu ni kuwa, mradi huu kiujumla wake umekamilika kwa asilimia 98.01,”.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji usambazaji Mhandisi Abubakar Issa amesema kwa sasa Tanzania hakuna kabisa mgao wa umeme kutokana na kuwa na ziada ya umeme.

“Mwisho wa mwezi huu tunatarajia kuingiza mashine namba saba ambayo itakwenda kuongeza megawati 235 na kupelekea kituo hichi kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 705,” amesema Mhandisi Issa.

Hii ni ziara ya kwanza ya bodi katika mradi huu ambapo imejionea hatua kubwa ya maendeleo ya ujenzi iliyofikiwa katika mradi huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here