Home KITAIFA WAZIRI SIMBACHAWENE ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE WIKI...

WAZIRI SIMBACHAWENE ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

📌 Wizara yatanabaisha miradi yake

📌 Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia waendelea kusambazwa

Dodoma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ambaye ni mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, ametembelea mabanda ya Wizara ya Nishati  na Taasisi zake katika Maadhimisho hayo yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Akiwa katika Banda la Wizara ya Nishati, Simbachawene alipokelewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Neema Mbuja ambaye alimweleza kuhusu miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na Wizara na ile inayotarajiwa kutekelezwa lengo kuu likiwa ni kuhakikisha nchi inakuwa na nishati ya kutosha kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo majumbani,  viwandani, magari na taasisi.

Aidha akiwa katika Banda la Wizara ya Nishati, Simbachawene ameelezwa kuhusu utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa  Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wanaachana na matumizi ya nishati isiyo safi  na kutumia nishati iliyo safi na salama.

Aidha, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Nishati, amemkabidhi Simbachawene nakala za Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha kuwa Mkakati huo unafika kwa makundi mbalimbali ya wananchi.

Viongozi wengine walioambatana na Simbachawene ni  Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais,  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe  Ridhiwan Kikwete na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here