Home KITAIFA VYOMBO VYA HABARI SIO MSHINDANI WA SERIKALI:DK. SAMIA

VYOMBO VYA HABARI SIO MSHINDANI WA SERIKALI:DK. SAMIA

Dar es Salaam

RAIS Dk. Samia suluhu Hassani amesema kuwa vyombo vya habari sio mshindani wa serikali bali ni mdau na ni mshiriki muhimu wa shughuli za serikali.

Pia Dk.Samia amesikitishwa na kifo cha mtoto mwenye Albino Asmiwe Novath mwenye umri wa miaka miwili na miezi sita ambae aliibwa mei 30 mwaka huu nyumbani kwao huko Muleba Mkoani Kagera na baadae kupatikana akiwa amefarikia dunia huku baadhi ya viungo vya mwili wake vikiwa vimenyofolewa.

Hayo ameyasema Leo Juni 18 jijijni Dar es Salaam Rais Dk. Samia wakati akifungua Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari na Kakao kazi cha Maafisa Habari wa Serikali lilohudhuliwa na viongozi mbalimbali na lilofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Mlimani City lenye kauli mbiu “jenga mustakabali endelevu kwenye sekta ya havari katika zama za kidijitali”.

Amesema serikali haina budi kuweka mifumo ya kisera na kisheria katika kuimarisha uhuru na mazingira ya vyombo vya habari na hiyo ndio kazi ambayo serikali inafanya hivi sasa.

“Huko nyuma kipindi fulani vyombo vya habari na serikali vilikuwa vinavutana na sisi tumevuta lakini tuliona hatutofika mahala hivyo tuliamua kukaa sehemu moja na kufanya kazi kwa pamoja,”amesema Rais Dk. Samia.

Amesema vyombo vya habari ni muhimu kulisemea Taifa mambo mazuri lakini kuna baadhi ya waandishi wahabari na vyombo vya habari vimekuwa vinqandika habari mbaya za kulitangaza vibaya Taifa lao pia amewakumbusha kuwa wazalendo kwa kuripoti habari za Taifa kwa weledi na kutangaza Mendeleo yaliyofikiwa.

“Nikienda huko nchi za wenzetu napongezwa kwa kazi nzuri inayofanywa kwa kusimamia sekta ya habari lakini wanahabari wenyewe wapo wasioona mazuri yanayafanywa na serikali,”amesema.

Aidha amesmea kuwa yeye ni muumini mzuri wa uhuru wanvyombo vya habari haamini kwenye kuminya uhuru wao kwa vyombo vya habari

Ameeleza kuwa vyombo vya habari vikiwa huru vinagusa kila pembe ya taifa na kuhamasisha kupokea ujuzi mpya, taarifa za maendeleo ya teknolojia, kufichua maouvu na kuutowajibika kunafanywa na watumishi na kusaidia viongozi kupata mrejesho

Amesema uhusiano kati ya serikali na vyombo vya habari unazidi kuimarika huku ripoti za kimataifa zikionesha kuimarika kwa uhuru wa Vyombo via habari nchidi.

Akizungumzia kuhusu madeni ya vyombo vya habari Rais Dk.Samia ameziagiza wizara na taasisi za umma kuhakikisha yanalipwa madeni hayo ifikapo Disemba mwaka huu.

“Wizara ya Fedha ihakikishe inapitia madeni haya yale yanayolipika yalipwe yenye ushaihidi na madeni ya vyombo vya habari yapewe kipaumbele, “amesema.

Dk.Samia amesema hakuna mfumo wa kibiashara hivyo vyombo vya habari viendeshwe kibiashara na sekta ya habari ni muhimu kukuza demokrasia.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye kongamano hilo amesema vipo vyombo vya habari vinafanya vizuri na kuitangaza Tanzania kwa kazi nzuri lakini kuna vingine hasa mitandao ya kijamii vimekuwa vikipotosha baadhi ya mambo.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye inagawa Tanzania haijafika katika uhuru wa habari inaoutarajia angalau ipo katika hatua tofauti na iliyokuwa siku za nyuma.

Amesema hilo ni mageuzi ya usimamizi katika sekta ya utangazaji na mapitio ya sera na kanuni ambayo misingi wake ni maelekezo ya Rais.

” Lengo la kongamano hili ni kutathmini sekta ya habari na kuweka mikakati tunakokwenda na kongamano hili ni la pili kufanyika kutakuwa na mada mbalimbali na kujadili kuondoka na maadhimio,”amesema Nnauye.

Amesema maboresho yaliyofanywa kwenye sekta ya habari ikiwemo na uhuru wa kujieleza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here