Home BIASHARA TADB WATANZANIA WANAWATEGEMEA KATIKA ELIMU NA MIKOPO – DK. BITEKO

TADB WATANZANIA WANAWATEGEMEA KATIKA ELIMU NA MIKOPO – DK. BITEKO

Pwani

NAIBU Waziri Mkuu Dk. Dotto Biteko amesema Watanzania wanawategemea katika uwezeshaji wa elimu na mikopo Banki ya maendeleo ya kilimo nchini TADB kwani Banki hiyo ndio zenye wajibu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kilimo Bora na ufugaji Bora wenye tija.

Amesema hayo Juni 16 wakati akikagua mabanda la maonyesho ya kibiashara la Bank ya Maendeleo ya Kilimo Nchini (TADB) alipofika Ubena Zomozi Halmshauri ya wilaya ya Chalinze mkoani Pwani kufunga maonesho ya tatu ya Wafugaji wa kibiashara yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wafugaji kibiashara nchini (TCCS).

Dk.Biteko amesema ameitaka TADB waendelee kutoa elimu na mikopo kwa Wafugaji nchini ili waweze kufuga kibiashara wapate tija katika ufugaji wao.

“Watanzania tunawategenea nyie, nyinyi ndio wenye wajibu mtubadilishe kutoka kwenye ufugaji tuliouzoea,” amesema Dk. Biteko.

Dk. Biteko amesema Wafugaji wamekuwa katika ufugaji wa asili kwa muda mrefu hivyo ili kubadilika inahitaji elimu ya ufugaji kibiashara ili na wao wakubali kubadilika na kuanza kufuga kibiashara.

“Wafugaji wanapitia changamoto nyingi hivyo hivyo msichoke kuwapa elimu ya ufugaji wa Kibiashara nina imani watabadilika taratibu na badaye nchi itakuwa na wafugaji wenye mifugo yenye faida.

“Msiwasahau wafugaji wanaofuga kienyeji na mwakani naomba baadhi wawepo kwenye maonesho haya kwani watakapokuja watajifunza na kubadilika,”amesema Dk. Biteko.

Amewataka wadau wezeshi hao kutoishia kwa wafugaji wa kibiashara bali wawafikie wafugaji wa kienyeji ili na wao waweze kuwa wafugaji wenye tija nchini kwani hilo ndilo lengo la serikali ya awamu ya sita ambayo inalenga kuwanyanyua wafugaji.

Aidha akizungumzia maeneo yaliyotengwa kwaajili ya shughuli za mifugo Naibu Waziri Mkuu huyo alizitaka Halmshauri za wilaya nchini kuhakikisha yanalindwa.

“Halmashauri za wilaya nchini zitunze maeneo ambayo yalitengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo,”amesema.

Serikali itaendelea kuunga mkono maonesho ya Wafugaji wa Kibiashara nchini ili waendeleze haya maonesho ambayo yanatoa elimu na kutoa Uhalisia wa ufugaji wa kibiashara utakaoongeza tija kwa wafugaji na kupata soko katika soko la kimataifa.

“Maonyesho haya muyapeleke katika ngazi za Kanda ambako yatakutana walengwa ambao ni wafugaji wa kienyeji na wawape elimu wabadilike na kufuga kibiashara,”amesema.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB David Nghambi amesema kuwa Benki hiyo kipindi cha miaka mitatu wametoa mikopo ya zaidi ya bilioni 13, wamewawezesha wafugaji kibiashara ili wawe na uhakika wa masoko kimataifa kwa kunenepa mifugo, pia wametoa mikopo ya bilioni 47 kwa wafanyabishara wa maziwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here