Home KITAIFA RAIS SAMIA ABAINISHA MIKAKATI YA TAARIFA YA MAPENDEKEZO YA TUME YA HAKI...

RAIS SAMIA ABAINISHA MIKAKATI YA TAARIFA YA MAPENDEKEZO YA TUME YA HAKI JINAI YAGUSIA MIHIMILI YOTE MITATU YA DOLA NA PANDE ZOTE MBILI ZA MUUNGANO

Dodoma

RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan amewapongeza na kuwashukuru Waziri Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) George Mkuchika na Jaji mstaafu Joseph Warioba ambao waliowaongeza katika kamati ya utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Haki jinai ambao kwa pamoja wameongeza chachu ya ziada kwakuwa wamekuwa na udhoefu wa muda mrefu.

Akizungumza kupitia hotuba yake, Rais Samia ameweka wazi kuwa kamati hiyo imeleta mikakati iliyoandaliwa kitaalamu zaidi kama ilivyotarajiwa ambapo amebainisha kuwa masuala yaliyomo yamejikita katika kugusa mihimili yote mitatu ya dola kwa maana ya Serikali, Bunge na Mahakama.

Vilevile, Rais Samia amesema mikakati hiyo ipo ya muda mfupi na muda mrefu ambayo yote kwa ujumla yake yatatelelezwa ndani ya miaka 5.

Aidha, Rais Samia amesema mikakati hiyo pia inagusia pande zote mbili ya Muungano (Tanganyika na Zanzibar).

Hayo yamejiri katika hafla fupi ya upokeaji wa Taarifa ya Kamati ya Kuunda Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai ambapo Rais Samia ameipokea kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here