Home BURUDANI WAZIRI NDUMBARO ASISITIZA WASANII KURASIMISHA KAZI ZAO .

WAZIRI NDUMBARO ASISITIZA WASANII KURASIMISHA KAZI ZAO .

Dar es Salaam

WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro amehimiza na kuwasisitiza wasanii kujiraismisha ili kurahisisha mipango ya Serikali ya kuwatafutia fursa mbalimbali kwa kuwa sanaa ni ajira inayoingiza kipato.

Dk.Ndumbaro ameyasema hayo Juni 14, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na watu mashuhuri katika hafla maalum ya kujadiliana mchango wao katika kujenga afya bora ya akili na maadili katika kazi za sanaa.

Amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imekuwa Mstari wa mbele kupambania maendeleo ya wasanii pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za kuendeleza Wasanii kiuchumi ikiwemo kufufua mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania ambao unawawezesha wasanii kufikia malengo yao ambapo hadi sasa umefanikiwa kutoa shilingi bilioni 4.2 kwa wasanii.

“Ndugu zangu wasanii tunapaswa kumshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mahaba anayoendelea kuyaonesha kwenye tasnia ya Sanaa kwani kupitia hotuba yake wakati wa tukio la uzinduzi wa albamu ya msanii Harmonize ametamka rasmi kuambatana na wasanii katika ziara zake ili kuwafungulia fursa za soko la Kimataifa,” amesisitiza Dk.Ndumbaro.

Mkutano huo maalum ulikuwa na mada mbalimbali zilizotolewa na wabobezi wa sekta ya sanaa na utamaduni ikiwemo mada ya usalama na uzalendo wa nchi, mikataba katika kazi za sanaa na uzingatiaji wa maadili katika kazi za sanaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here