Home KITAIFA JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA BINTI WA MIAKA 14 WILAYANI MASWA

JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA BINTI WA MIAKA 14 WILAYANI MASWA

Na Shomari Binda-Maswa

MAHAKAMA ya Hakimu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imemtia hatiani mshitakiwa Beatus Manon mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa Kijiji cha Zanzui kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 14.

Hukumu hiyo imetolewa leo Juni, 14 2024 kufuatia shauri la jinai bamba 6386/2024 katika Mahakama ya wilaya ya Maswa mbele ya Hakimu Azizi Mzee Khamis.

Mshitakiwa huyo alishitakiwa katika Mahakama ya wilaya ya Maswa kwa kosa moja ambalo ni kubaka kinyume na kifungu cha 130 (1)(2)(e)na 131 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2022 .

Awali Mahakamani hapo inadaiwa na mwendesha mashtaka kutoka ofisi ya taifa ya Mashtaka wilaya ya Maswa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Vedastus Wajanga kuwa tarehe 1 mwezi januari 2024 majira ya saa 12 za jioni katika Kijiji cha Zanzui ndani ya wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu mshitakiwa alimbaka muhanga mwenye umri wa miaka 14 ambaye jina lake limeifadhiwa kwa kumvuta kwa nguvu na kumpeleka vichakani pindi muhanga alipokuwa anatoka maeneo ya centre ya Zanzui akielekea nyumbani kwao.

Taarifa zilifika kituo cha polisi ambapo mshtakiwa alikamatwa na alipohojiwa kituoni kwa kuandikwa maelezo yake ya onyo alikana kutenda kosa hilo na baada ya upelelezi kukamilika mshtakiwa alifikishwa Mahakamani

Jumla ya mashahidi 6 na kielelezo kimoja ulitolewa na upande wa mashtaka a
baada ya ushahidi huo mshtakiwa alijitetea kwa kusema hana la kujitetea.

Upande wa mashtaka uliomba mshitakiwa apewe adhabu Kali ili iwe funzo kwake na kwa jamii kwani makosa ya kubak yanaongezeka katika jamii na yanaleta athari kubwa Kwa muhanga kisakolojia na kijamii , kichumu pamoja na kiafya ukizingatia kuwa mshtakiwa ni kijana ambae ana uwezo wa kumchumbia binti au mwanamke yoyote ambae hayupo chini ya umri wa miaka 18.

Ulidai pia makosa kama haya ni ukatili wa kijisia katika jamii na hatimae huweza kusababisha maradhi au kifo Kwa muhanga.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Azizi Mzee Khamis alimuhukumu mshitakiwa kifungo cha miaka 30 jela na faini ya shilingi 300,000/=kwa mhanga huku haki ya rufaa ikiwekwa wazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here