Home KITAIFA RAIS WA CHAMA CHA TAS ALILIA HUKUMU KALI KWA WANAOKUTWA NA VIUNGO...

RAIS WA CHAMA CHA TAS ALILIA HUKUMU KALI KWA WANAOKUTWA NA VIUNGO NA MAUAJI YA ALBINO NCHINI

Pwani

RAIS wa Chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Godson Mollel aonyesha kushangazwa na Mahakama nchini kutowahi kutoa adhabu kali kwa watu wanaokutwa na hatia ya kuwakata viungo au kuwaua watu wenye Ualbino.

Amesema hayo Juni,11, 2024 mjini Kibaha wakRais huyo wa Chama cha Watu wenye ualbino nchini TAS Godson Mollel alipozungumza na Waandishi wa Habari siku ya kwanza ya Maadhimisho ya kitaifa ya siku kuongeza uelewa juu ya Ualbino (IAAD) duniani ambayo kitaifa yanefanyika Kibaha mkoani Pwani

Mollel amesema kuwa Mahakama ikitoa hukumu kali kwa wahusika hao itakuwa fundisho kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha kuwadhuru watu wenye Ualbino itakuwa funzo kwa wenye tabia hizo.

Naye ofisa Ustawi Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Watu wenye ulemavu Joy Maongezi amesema kuwa sheria namba 9 ya mwaka 2010 inataka kuwa na haki kwa watu wenye ulemavu ambapo watu wenye Ualbino ni sehemu yao.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Shangwe Twamala amesema wakati wa maadhimisho hayo huduma mbalimbali zinatolewa ikiwa ni pamoja na upimaji saratani ya ngozi, utoaji miwani, kofia na losheni ya kuzuia ngozi kuathirika, upimaji wa tezi dume na kansa ya kizazi.

Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka duniani ambapo kilele huwa Juni,13 2024 kila mwaka na kwa mwaka huu kitaifa yanafanyika Kibaha Mkoani Pwani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here