Home KITAIFA MATOKEO YA UWEKEZAJI TPA YAVUNJA REKODI YA KUTOA GAWIO LA SHILINGI...

MATOKEO YA UWEKEZAJI TPA YAVUNJA REKODI YA KUTOA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 153.9 SERIKALINI

Dar es Salaam

IKIWA ni miezi michache tu imepita mara baada ya maboresho ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni mbili za kimataifa katika Bandari ya Dar es Salaam, tayari uwekezaji huo umeshazaa matunda.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imevunja rekodi kwa kutoa jumla ya Shilingi za Kitanzania bilioni 153.9 kama gawio kwa Serikali kuu kwa mwaka wa fedha Mwaka 2023/2024.

Gawio hilo limeifanya TPA, kuongoza kwa kutoa gawio kubwa zaidi kuliko taasisi zote za Serikali hapa nchini,

“Haya ni matunda ya uwekezaji uliofanywa katika Bandari ya Dar es Salaam,”amasema Mkurugenzi Mkuu, BPrasduce Mbossa.


TPA imefanya uwekezaji mkubwa kwa kuboresha miundombinu ya kwa Bandari zake. Katika Bandari ya Dar es Salaam, TPA imefanya maboresho ya ujenzi wa magati na kuongeza kina, imetanua lango la kuingilia Bandarini na sehemu ya kugeuzia meli.

Mamlaka pia imekuwa ikishirikiana na vyema kiutendaji na wawekezaji ambapo hadi sasa Kampuni ya DP World imeshafanya uwekeza mkubwa kwa kununua vifaa kama SSGR (Ship to Shore Gang Cranes) nane (8), pamoja na T.T. (Terminal Tractors) 50.

Ushirikiano huo umefanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa ya kisasa, kuongeza ufanisi na kutoa huduma zake za kuhudumia meli na mizigo kwa ubora na ufanisi zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here