Home KITAIFA BRELA YATOA GAWIO KWA SERIKALI KWA TAASISI ZA UMMA

BRELA YATOA GAWIO KWA SERIKALI KWA TAASISI ZA UMMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan jana Juni, 11 2024, amepokea gawio la kiasi shilingi Bilioni Kumi na Nane Mia Tisa Sabini na Tatu, Millioni Mia Nane Hamsini na Tatu Elfu, Mia Tano Kumi na Nne na Senti Ishirini na Saba tu (18,973,853,514.27) kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), ikiwa ni utekelezaji wa utoaji gawio  kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Sheria ya Msajili wa Hazina Sura 370. Hafla hiyo imehudhuriwa na Dkt Fred Msemwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Waziri kwa BRELA na Bw Godfrey Nyaisa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here