Morogoro
WATUMISHI wa Kurugenzi ya Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, wamepigwa msasa namna ya kudhibiti utoroshaji wa madini nje ya nchi na kuikosesha serikali mapato.
Mafunzo hayo yametolewa leo Juni 10, 2024 na Wataalam kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye Ofisi za Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro. Pia, wamepatiwa mafunzo ya kodi katika ‘Capital Asset na Capital Gain’.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na kuboresha utendaji kazi.