Zanzibar
RAIS Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi M Dk. Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Taasisi ya Al Mazrui Charitable Organisation ya Abu Dhabi kwa kuendelea kutoa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo afya , elimu na maji.
Pia ameishukuru taasisi hiyo kwa kutoa jengo lao kwa Serikali ilitumie kwa huduma za afya.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo akizungumza na vijana wa Chuo cha ufundi Mubarak AL Mazrui na alipotembelea eneo hilo Mkoa wa Mjini Magharibi Juni 11 2024.
Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali imetoa kibali cha kuajiri vijana waliokuwa wanajitolea katika mashirika mbalimbali ya Serikali ikiwemo Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA).